Description
lliyokuwa safari ya kawaida ya likizo mashambani kuzuru Babu na Nyanya ilibadilika na kuwa safari yenye mafunzo na
uvumbuzi tele kwa Lamudimu na Nilinde. Wanajifunza kuhusu kulinda mazingira, utamaduni na jinsi ya kuishi vyema na wenzao.
Wanaapa kwenda kuwafundisha wenzao mjini umuhimu wa kwenda mashambani na pia wao wenyewe kurudi mashambani tena katika
likizo nyingine ili wafurahie vituo zaidi vya kitalii kama mwamba wa jiwe linalolia la Khayega na kupigana kwa mafahali.
Je, wanagundua sababu za jiwe kulia? Watarudi kwa likizo nyingine tena?






