Description
Matatizo ya chombo baharini yanapelekea Sudana, msafiri mkembe, pamoja na jamaa yake kujikuta dhidi ya washirika wawili – Amerigo na Muzungu, watu ambao matendo, tabia na hatua zao zinatawaliwa na imani, mielekeo na taasubi kali. Anatatizika baina ya kulinda hadhi yake, kwa upande mmoja na kuiuza hadhi hiyo, kwa upande mwingine, ili kuwanusuru wanawe wasiangamizwe katika madhila na mzigo wanaotwikwa na Amerigo na mshirika wake. Maingiliano changamano baina ya pande hizi mbili ndiyo yanayosuka hadithi ya tamthilia hii.
Prof. Alamin Mazrui ni mwalimu na mwandishi maarufu. Baadhi ya kazi zake zilizochapishwa ni Kilio cha Haki (tamthilia Longhorn) na Chembe cha Moyo (Ushairi).
Prof. Kimani Njogu ana tajriba pana ya ufundishaji wa lugha na fasihi ya Kiswahili. Baadhi ya vitabu vyake vilivyochapishwa ni Mwongozo wa Siku Njema na Mwongozo wa Amezidi vilivyochapishwa na Longhorn. Aidha, Prof. Njogu ni mshindi wa tuzo ya NOMA mwaka 2000 kupitia kitabu chake Ufundishaji wa Fasihi: Mbinu na Nadharia.






