Description
Hekaya za Abunuwas na Hadithi Nyingine ni mkusanyo wa hadithi za kusisimua. Hadithi zilizomo zimesimuliwa kwa ucheshi wa hali ya juu. Hadithi hizi, vilevile, zina mafunzo muhimu ambayo yatamwongezea maarifa msomaji. Maadili yametukuzwa huku ujinga na maovu yakitwezwa. Yeyote anayependa kusoma hadithi za Kiswahili atafurahia kuwa na nakala ya kitabu hiki.






