Description
Sifa ya kubana mambo na matukio, mwondoko wa haraka haraka wa hadithi, kuzuia na kudokeza kidogo kidogo kwa yanayotokea kwa maana ya taharuki na hadithi hatimaye kuishia mwanguko wa mshangao, ni mbinu muhimu za hadithi fupi yoyote ile. Na bila ya shaka ukwasi wa lugha. Hadithi zilizomo kwenye mkusanyo huu wa Said A. Mohamed, zinatimiliza sifa zote hizi. Na zaidi zimo katika maudhui mbalimbali yanayozunguka kwenye mapenzi, chuki, ukweli, udanganyifu, ubinadamu na unyama, mwelekeo wa nchi zetu kisiasa, mwanamke na mwanamume katika husiano zao mbaya na nzuri na hatimaye, furaha na misiba. Kwa jumla msomaji hatakiwacha kitabu hiki kukisoma mara anapoanza kukikamata.






