Description
“…. Baada ya kuyaona hayo, bado unataka kuwa muuguzi?” Rafiki yake Kido alimwuliza. “Ndiyo, nitafanya juu chini niwe muuguzi kama Shangazi Mela au Daktari Machizi,” Kombo alimjibu kwa imani…. Sifa zipi zilimfanya Kombo kutimiza ndoto yake? Soma upate jibu. Vitabu vya Adili vimekusudiwa kuburudisha na kuelekeza. Kitabu hiki kimependekezwa kwa madarasa ya juu katika shule za msingi.






